Ingawa kampuni hiyo (SAR) iliundwa mwaka 1961, ni mara ya kwanza inasafisha mafuta yanayozalishwa nchini, hadi sasa ilikuwa inasafisha tu mafuta yanayoagizwa nje.
SAR “ina fahari ya kutangaza kwamba imefaulu kusafisha mafuta ghafi ya kwanza yanayozalishwa nchini Senegal huko Sangomar”, jina la eneo la uzalishaji wa mafuta katika pwani ya magharibi mwa Senegal, kampuni hiyo ilisema katika taarifa.
Kampuni hiyo ilisema imesafisha mapipa 650,000 ya mafuta ghafi tangu siku ya Jumamosi, ambayo nayo yamezalisha tani 90,000 za bidhaa tofauti, ikiwemo dizeli, mafuta ya taa, petroli na gesi ya butane.
Forum