Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 05:13

Kesi 82 za madai ya watu kutoweka nchini Kenya zimeripotiwa tangu June 2024


Bendera ya Kenya
Bendera ya Kenya

Watu wengi wanatuhumu polisi kwa kufanya vitendo hivyo lakini bado haijathibitishwa ni nani aliyehusika na utekaji huo.

Tangu Juni 2024 wakati mfululizo wa maandamano makubwa ulipofanyika nchini Kenya kesi 82 za madai ya watu kutoweka kwa kulazimishwa zilirekodiwa na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Kenya.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waathirika wa tukio hilo wamepata bahati ya kuungana tena na wapendwa wao lakini 29 bado hawajulikani walipo.

Huku wengi wanatuhumu polisi kwa kufanya vitendo hivyo, lakini bado haijathibitishwa ni nani aliyehusika na utekaji huo. Aslam Longton na kaka yake Jamil, waliiambia VOA kuwa walitekwa nyara karibu na nyumba yao katika kitongoji cha Kitengela Town kiasi cha saa moja kutoka katikati mwa Nairobi.

Mapema siku hiyo hapo Agosti, Aslam alisema alihisi wasiwasi na aliona watu wasiojulikana wakiangalia kila hatua anayofanya. Ndugu hao walikuwa Pamoja ndani ya gari wakati tukio hilo lilipowakuta.

Forum

XS
SM
MD
LG