Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance aliongoza Mkutano wa Siasa wa kihafidhina na vikao vingine muhimu vinavyohusu Cryptocurrency
Viongozi wa Taliban wenye msimamo mkali nchini Afghanistan, wamekataa mamlaka ya mahakama ya uhalifu wa kimataifa ICC nchini humo, na kutangaza hatua ya waliokuwa viongozi wa nchi hiyo kuingiza Afghanistan katika makubaliano ya ICC mwaka 2003, kuwa kinyume cha sheria.
Maelfu ya watu hawana umeme katika mji wa Odesa, kusini mwa Ukraine, kufuatia mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa na Russia.
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba makubaliano ya kibiashara yanaweza kupatikana kati ya Marekani na China.
Wanamgambo wa Hamas wameachilia miili ya waisrael wanne, na kusafirishwa kwa msafara wa magari ya shirika la msalaba mwekundu kutoka Khan Younis, kusini mwa Gaza.
Serikali ya Kenya imkosolewa na mkuu wa jeshi la Sudan na baadhi ya wakosowaji wa nchi hiyo kwa kudai imefanya kitendo cha uhalifu wa kutowajibika kwa kuwaruhusu waasi wa kundi la wanamgambo wa Sudan RSF kukutana Nairobi na kupanga kutangaza serikali ya uhamishoni.
Wahandisi wa kijeshi wa Marekani wamelenga zaidi ya miradi 600 ya nishati na miundombinu ambayo inaweza kuharakishwa chini ya mpango wa kitaifa wa Dharura ya Nishati uliotangazwa na Rias Donald Trump, kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti yao.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth ameomba baadhi ya vitengo vya jeshi kupendekeza matumizi yatakayo punguzwa kama sehemu ya punguzo la asilimia 8 ndani ya kila mwaka kwa miaka 5 mitano ijayo.
Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO Jumatano limesema kuwa mazungumzo kususu taharuki za kibiashara ni muhimu baada ya China kutuhumu Marekani kwa hatua ya kuongeza ushuru, inayoweza kuyumbisha soko la kimataifa.
Mwanamke wa Kiyazidi aliyenusurika ubakaji na kuzuiliwa na kundi la Islamic State huku akiokolewa kutoka Gaza Oktoba mwaka jana kupitia operesheni iliyoongozwa na Marekani, hatimaye amewasili Ujerumani.
Marekani imeongeza maradufu idadi ya wafungwa wanaodhaniwa kuwa tishio kubwa pamoja na wale wanaosubiri kurejeshwa makao kwenye kituo cha jeshi la wanamajaji la Marekani cha Guantanamo Bay nchini Cuba.
Mashambulizi kutoka kwa kundi la kijeshi la Rapid Support Forces la Sudan yameua mamia ya raia wakiwemo watoto, kwenye jimbo la White Nile, maafisa wa serikali na makundi ya haki za binadamu wamesema Jumanne.
Pandisha zaidi