Wafanyakazi wa huduma za dharura zikiwemo boti na wapiga mbizi walifanya kazi kwenye mto Potomac kuokoa abiria
Ndege ya abiria iligongana na helikopta ya kijeshi ya Marekani Jumatano usiku wakati ilipokuwa inakaribia kutua kwenye uwanja wa ndege wa Washington DC Reagan National, Mamlaka ya usafiri wa anga FAA ilisema.
Jaji Jumatano amemhukumu seneta wa zamani wa Marekani mwenye ushawishi mkubwa kifungo cha miaka 11 jela, baada ya kukutwa na hatia ya rushwa kufuatia kugunduliwa kwa dhahabu nyingi na maelfu ya dola pesa taslimu nyumbani kwake.
Jumuia ya Afrika Mashariki Jumatano imeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzungumza na “wadau wote”, wakiwemo wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda, ili kumaliza mapigano katika eneo la mashariki mwa nchi.
Kundi la waasi wa M23 limesonga mbele kwenye uwanja mwingine wa mapambano huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa kuteka wilaya mbili katika jimbo la Kivu Kusini, vyanzo vya eneo hilo vimeiambia AFP Jumatano.
Sehemu kubwa ya mji uliokumbwa na mzozo wa Goma zilikuwa shwari mapema Jumatano asubuhi, baada ya siku ambayo maelfu ya watu waliokuwa wakikimbia walijificha kando ya barabara.
Kesi iliwasilishwa Jumanne kwenye mahakama ya serikali kuu jijini Washington kwa niaba ya mashirika yasiyo ya faida, wamiliki wa biashara ndogo ndogo na wataalamu wa afya ya umma, saa chache kabla ya amri ya kusitishwa kwa fedha za ufadhili wa serikali kuu kuanza kutekelezwa.
Maelfu ya watu katika nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zinazoongozwa na serikali za kijeshi Jumanne waliandamana kuunga mkono uamuzi wa nchi hizo wa kujiondoa kwenye Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Kundi la waasi wa M23 Jumanne lilichukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa mji wa Goma, chanzo cha usalama kimesema, kufuatia mapigano ya siku tatu ambayo yameua zaidi ya watu 100.
Waziri wa Mambo wa Nje wa Marekani Marco Rubio Jumanne amezungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Mapigano makali yanaendelea kati ya wanajeshi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na wapiganaji wa kundi la waasi la M23 wanaoungwa mkono na wanajeshi wa Rwanda, katika mji wa Goma.
Mamlaka nchini Sudan Kusini imeondoa marufuku ya muda ya mitandao ya kijamii ya Facebook na TikTok, ambayo iliwekwa wiki iliyopita kufuatia kusambazwa kwa video zilizoonyesha madai ya mauaji ya raia wa Sudan Kusini nchini Sudan.
Pandisha zaidi