Serikali ya kijeshi ya Myanmar imewaachia huru zaidi ya wafungwa 6,000 na kupunguza adhabu za vifungo vya wafungwa wengine, kama sehemu ya msamaha kwa watu wengi katika kuadhimisha miaka 77 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza siku ya Jumamosi.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika mahojiano yaliyochapishwa Jumamosi , amelaani matamshi “ ya ovyo ” ya Elon Musk na msimamo wake wa wazi kukiunga mkono chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD.
Wizara ya ulinzi ya Russia Jumamosi imesema wanajeshi wa Russia wamedhibiti kijiji cha Nadiya katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Luhansk na kutungua makombora manane yaliyotengezwa Marekani aina ya ATACMS.
Wizara ya afya ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu imesema mtu mmoja aliuawa na wengine tisa kujeruhiwa katika shambulio la Israel kwenye kambi ya wakimbizi, huku jeshi la Israel likisema Jumamosi kwamba limewafyatulia risasi “magaidi.”
Watu wenye silaha kutoka Nigeria wamewaua wanajeshi watano wa Cameroon na kuwajeruhi wengine kadhaa katika kijiji cha Bakinjaw kwenye mpaka wa Cameroon na Nigeria, mbunge wa wilaya alisema Jumamosi.
Rais wa Ghana anayeondoka madarakani Nana Akufo Addo Ijumaa ametangaza kuwa watu wote wenye passpoti za Afrika kuanzia mwaka huu wataingia nchini humo bila ya visa, hatua inayoashiria kuelekea muingiliano wa kiuchumi barani Afrika.
Waziri mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra Ijumaa alitangaza mali zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 400, chama chake kimesema, ikijumuisha zaidi ya mikoba ya mkononi 200 iliyotengenezwa na wabunifu yenye thamani ya dola milioni 2 na saa 75 za kifahari zenye thamani ya dola milioni 5.
Mamlaka za Korea Kusini Ijumaa zimesimamisha jaribio la kumkamata Rais aliyeondolewa baada ya kushtakiwa na bunge Yoon Suk Yeol kufuatia hali ya mvutano mkali wa saa sita kati ya wachunguzi na maafisa wa usalama watiifu kwa rais huyo.
Jeshi la Israel limeripoti kwamba limetungua kombora na ndege isiyokuwa na rubani iliyorushwa Ijumaa kutoka Yemen, ukiwa msururu wa mashambulizi ya hivi karibuni kutoka nchini humo kuilenga Israel katika wiki za hivi karibuni.
Wahamiaji 27 wakiwemo wanawake na watoto, walifariki wakati boti mbili zilipopinduka kwenye pwani katikati mwa Tunisia, huku watu 83 waliokolewa, afisa wa ulinzi wa kiraia aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi.
Waandamanaji kadhaa walikusanyika katika mji wa Douma nchini Syria, Jumatano kudai majibu katika kutoweka kwa wanaharakati wanne mashuhuri waliotekwa nyara zaidi ya muongo mmoja uliopita.
Dereva mmoja aliendesha gari kwenye umati wa watu waliokuwa wakisherehekea Mwaka Mpya, Jumatano mapema mjini New Orleans na kufyatua risasi, na kuuwa watu 10 pamoja na kujeruhi wengine zaidi ya 35 katika shambulizi FBI imesema inachunguza kama kitendo cha kigaidi.
Pandisha zaidi