Abiria waliookolewa na kufariki, waligundulika kwenye visiwa vya Kerkennah karibu na katikati mwa Tunisia, wakiwa njiani kuelekea Ulaya, wakitokea katika nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika, amesema Zied Sdiri, mkuu wa ulinzi wa kiraia katika mji wa Sfax.
Msako ulikuwa unaendelea kwa uwezekano wa kuwapata abiria wengine ambao hawajapatikana, kwa mujibu wa Kikosi cha Taifa cha Ulinzi cha Tunisia, ambacho kinasimamia ulinzi wa pwani.
Tunisia ni kituo kikuu cha kuondokea kwa wahamiaji ambao wanataka kufika Ulaya kupitia Italy, ambako wanafika katika kisiwa cha Lampedusa kiasi cha kilometa 150 kutoka Tunisia, mara nyingi hicho ndiyo kituo chao cha kwanza.
Kila mwaka, maelfu ya watu wanajaribu kutumia njia hatari ya kuvuka bahari ya Mediterranean, ambayo inaonekana kujaa boti chakavu, huku kukiwa na hatari zilizochangiwa na hali mbaya ya hewa.
Hapo Desemba 18, takriban wahamiaji 20 kutoka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara walifariki katika ajali ya boti kwenye mji wa Sfax.
Forum