Kimbunga hicho kiliwasili mji wa pwani wa Pemba katika jimbo la kaskazini la Msumbiji la Cabo Delgado, na kuleta mvua na upepo mkali siku ya Jumapili.
Video iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto UNICEF, inaonesha boti zilizoharibiwa kwenye ufukwe wa mji huo pamoja na kuharibika nyumba na kuanguka kwa miti.
Msemaji wa UNICEF nchini Msumbiji, Guy Taylor anasema kiwango kamili cha uharibifu hakijulikani bado lakini miji na vijiji vitakumbwa na tatizo la ukosefu wa shule na huduma za afya kwa muda usiojulikana.
Kabla ya kuwasili Msumbiji kimbunga Chido kilisababisha hasara kubwa katika kisiwa cha kinacho tawaliwa na Ufaransa cha Mayotte siku ya Jumamosi, na idadi ya vifo inasemekana huwenda ikafikia zaidi ya mia moja kulingana na maafisa wa huduma za dharura katika kiswa hicho.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameahidi msaada kwa wakazi wa Maore alipokutana na Papa Francis kwenye uwanja wa ndege wa Ajaccio, mjini Corsica Ufaransa.
Idadi rasmi wa watu walofariki kwenye kisiwa hicho ni 14, lakini mkuu wa mkoa Francois-Xavier Bieuville anasema huwenda idadi ikapindukia mamia ya vifo kwa sababu kuna wahamiaji wengi wasio na vibali ambao hawajandikishwa kisiwani humo.
Ameongezea kusema kwamba kwa vile wakazi wa Mayotte ni waislamu watazika katika kipindi cha saa 24 na hivyo huwenda ikawa vigumu kujua idadi halisi ya vifo.
Forum