Alitangaza hayo katika hotuba yake ya mwisho kwa taifa wakati akijiandaa kuachia ngazi Januari 6 baada ya mihula miwili madarakani.
“Ni fahari kwangu kuidhinisha usafiri bila visa kuingia Ghana kwa Waafrika wote wenye hati za kusafiria kuanzia mwaka huu,” Akufo Addo alisema katika hotuba yake kwenye bunge.
“Haya yote ni mambo muhimu katika utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Afrika ya 2063, ambayo inalenga kuwa na Afrika yenye ushirikiano na iliyoungana ifikapo mwaka 2063,” aliongeza, akimaanisha mpango wa maendeleo wa Umoja wa Afrika kwa kipindi cha miaka 50.
Ghana imejiunga na Rwanda, Ushelisheli, Gambia na Benin kwa kuwaruhusu wasafiri wa Kiafrika kuingia nchi hizo bila visa.
Forum