Amekuwa kizuizini katika mji mkuu wa Kampala tangu alipokamatwa Novemba 2024 akiwa na msaidizi Obeid Lutale.
Rais wa zamani wa Nigeria Chifu Olusegun Obasanjo amefanya ibada ya ukumbusho huko Abeokuta kusini magharibi mwa Nigeria kwa heshima ya Rais zamani wa Marekani Jimmy Carter ambaye alifariki decemba 29 na kuzikwa wiki iliyopita.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Jumapili alisema kwamba Kyiv iko tayari kuwakabidhi wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini kwa kiongozi wao Kim Jong Un ikiwa atarahisisha ubadilishanaji wao na Waukraine wanaoshikiliwa mateka nchini Russia.
Chama tawala nchini Chad kimepata viti vingi katika uchaguzi wa bunge wa mwezi Disemba, ambao ulisusiwa na vyama vikuu vya upinzani ambapo wachambuzi wanasema utaimarisha nguvu za kisiasa za rais, matokeo ya awali yameonyesha.
Comoros Jumapili ilipiga kura kuwachagua wabunge, huku makundi mengi ya upinzani yakisema yatasusia uchaguzi huo ambao wanadai hauna uwazi.
Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Tanzania alitekwa nyara Jumapili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, na kuachiliwa baadaye baada ya makundi ya haki za binadamu kuingilia kati kwa haraka.
Wanadiplomasia wakuu wa Mashariki ya Kati na Ulaya, Jumapili wamewasili katika mji mkuu wa Saudi, kujadili Syria, huku mataifa yenye nguvu duniani yakishinikiza kuwepo utulivu baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad.
Sweden itachangia meli tatu za kivita katika juhudi za NATO kuongeza uwepo wa muungano huo katika bahari ya Baltic wakati inajaribu kulinda dhidi ya uharibifu wa miundombinu ya chini ya bahari, serikali imesema Jumapili.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, Jumapili ametoa wito kwa washirika wake kuheshimu ahadi zote za kuipatia Ukraine silaha, zikiwemo zile za kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Russia.
Nayo wizara ya Ulinzi ya Russia imesema iliingilia kati na iliharibu ndege zisizokuwa na rubani 85 za Ukraine usiku wa kuamkia leo.
Msafara huo ulitoka kutoa pole ya msiba kwa mwenzao ulishambuliwa na majambazi msemaji wa polisi alisema.
Ni baada ya mivutano juu ya mipango ya Addis Ababa kujenga kambi ya jeshi la majini katika mkoa wa Somalia uliojitenga.
Pandisha zaidi