Polisi wa kundi la Palestina la Hamas walionekana wakishika zamu nje ya jengo la makao makuu yao lililoharibiwa katika mji wa Gaza City Jumatano baada ya makubaliano ya sitisho la mapigano baina ya Hamas na Israel kuanza kutekelezwa.
Maelfu ya watu wameuwawa na wengine zaidi ya milioni 12 wamekoseshwa makazi kutokana na mzozo uliozuka baina ya jeshi la Sudan na kundi la waasi tangu April mwaka 2023.
Nchi tatu zinazotawaliwa na wanajeshi katika kanda ya Sahel zitaungana kuunda kikosi cha wanajeshi 5,000 kupambana na ghasia za wanajihadi ambazo zimekumba mataifa hayo kwa miaka kadhaa, maafisa walisema Jumanne.
Maafisa wa Uturuki wamesema Jumanne kwamba moto kwenye hoteli yenye ghorofa 12 katika mji maarufu wa kitalii kaskazini magharibi wa nchi umeua takriban watu 76, wawili miongoni mwao wakiwa ni kutokana na kuruka kutoka jengo hilo baada ya moto kuzuka.
Makundi ya Wakurdi nchini Syria yameelezea matumaini yao kwamba Marekani itaendelea kuwaunga mkono wakati rais mpya Donald Trump anapoanza kuhudumu kwenye muhula wa pili.
Miongoni mwa amri za kiutendaji zililenga uhamiaji kama vile kutangaza hali ya dharura kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.
Rubio ameanza kazi akiwa mwenyeji wa mkutano na wenzake kutoka Australia, India na Japan.
Vizuizi haviongozi mahala popote na hakuna mshindi katika vita vya kibiashara, anasema Makamu wa Waziri Mkuu wa China, Ding
Akizungumza baada ya kula kiapo kama rais wa 47 wa Marekani siku ya Jumatatu Januari 20, 2025, ndani ya ukumbi wa Rutanda katika jengo la bunge, Rais Trump amesema ataleta mapinduzi katika maisha ya Wamarekani.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Jumatatu alithibitisha uwepo wa mlipuko hatari wa virusi vya Marburg kaskazini magharibi mwa nchi, huku kesi nyingine moja ya ugonjwa huo ikiripotiwa.
Viongozi mbali mbali wa mataifa Jumatatu wameendelea kumpongeza rais mpya wa Marekani Donald Trump, kufuatia kuapishwa kwake kama rais wa 47.
Rais mpya wa Marekani Donald Trump Jumatatu usiku baada yakuapishwa mchana alikutana na maelfu ya wafuasi wake kwenye ukumbi wa Capitol One Arena mjini Washington DC.
Pandisha zaidi