Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 07:50

Zelenskyy na Netanyahu wampongeza Trump muda mfupi baada ya kuapishwa


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Viongozi mbali mbali wa mataifa Jumatatu wameendelea kumpongeza rais mpya wa Marekani Donald Trump, kufuatia kuapishwa kwake kama rais wa 47.

Miongoni mwa viongozi hao ni rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy. “Rais Trump ni mtu mwenye kauli, na amani kupitia sera ya nguvu aliyotangaza inatoa nafasi ya kuimarisha utawala wa Marekani pamoja na upatikanaji wa amani ya kudumu ambayo ni kipaumbele,” Zelenskyy alisema.

Hapo nyuma Trump aliahidi kumaliza vita vya Russia na Ukraine kwa siku moja baada ya kuchukua madaraka au hata kabla. Hata hivyo katika siku za karibuni washauri wa wake wamesema kuwa kutatua mzozo huo huenda kukachukua miezi kadhaa.

Trump hapo nyuma alitilia mashaka kuhusu kuendelea kwa Marekani katika kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pia alitoa pongezi zake kwa Trump, akisema kuwa “ Naamini kwamba kufanya kazi pamoja kutaimarisha ushirikiano kati ya Marekani na Israel hata zaidi.”

Sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas lilianza kufanya kazi Jumapili siku moja tu kabla ya Trump kuapishwa. Miongoni mwa viongozi wengine waliompongeza Trump ni pamoja na Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte na kiongozi wa EU Ursula von der Leyen, pamoja na mataifa shirika kama vile Ujerumani, Italy na Uingereza.

Forum

XS
SM
MD
LG