Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:56

Trump atia saini amri kadhaa za kiutendaji saa chache baada ya kuapishwa


Picha ya maktaba ya Trump akitia saini amri ya kiutendaji. January 20, 2025. (Photo by Jim WATSON / POOL / AFP)
Picha ya maktaba ya Trump akitia saini amri ya kiutendaji. January 20, 2025. (Photo by Jim WATSON / POOL / AFP)

Rais mpya wa Marekani Donald Trump Jumatatu usiku baada yakuapishwa mchana alikutana na maelfu ya wafuasi wake kwenye ukumbi wa Capitol One Arena mjini Washington DC.

Trump alichukua nafasi hiyo kuwajulisha kwa familia yake pamoja na makamu wake JD Vance, huku akitia saini amri kadhaa za kiutendaji na kusema kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahamiaji haramu.

Trump pia alisema kuwa wafanyakazi wote wa serikali ni lazima wafanyie kazi kwenye ofisi zao. Amri nyingine ya kiutendaji inatoa idhini kwa mawaziri wake kuchukua kila hatua kukabiliana na mfumuko wa bei za bidhaa na hasa vyakula.

Pia alisesema kuwa Marekani itaondoka mara moja kwenye mkataba wa hali ya hewa wa Paris, wakati pia akilalamikia ukosefu wa usawa wa kibiashara na China.

Forum

XS
SM
MD
LG