Madini muhimu na mafuta, na kushuka kwa ushawishi Magharibi kwenye ukanda wa Sahel, ni baadhi ya sababu ambazo wachambuzi wanaamini waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, amezichagua Jamhuri ya Congo, Nigeria, Chad na Namibia kama vituo vyake vya kwanza wakati wa ziara yake ya Afrika wiki hii.