Kwa miongo mingi, umekuwa ni utamaduni kwamba mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Beijing huwa akifanya ziara yake ya kwanza ya kimataifa barani Afrika, na kila wakati, wataalamu hujaribu kuchambua sababu za chaguo kwa mataifa yanayotembelewa.
“Mara nyingi unakuwa mchanganyiko wa mataifa makubwa na madogo. Sababu kubwa ya hayo yote ni kuonyesha kwamba China ni mshirika asiyebagua, na kwamba kila nchi ni sawa, kinyume na mataifa ya Magharibi ambayo hubagua,” amesema Cobus van Staden mhariri kutoka China Global South Project, wakati akizungumza na VOA kupitia ujumbe wa WhatsApp.
Wakati wa ziara yake ya kwanza huko Namibia Jumatatu, Wang alisema kuwa utamaduni wa miaka 35 wa kuanza na ziara ya Afrika, unauonyesha ulimwengu kwamba China imebaki kuwa rafiki wa Afrika wa kutegemewa zaidi, na pia mshirika mwenye nguvu zaidi kwenye jukwaa la kimataifa,” shirika la habari la serikali ya China la Xinhua limeripoti.
Forum