Wizara haijatoa maelezo kuhusu ni vituo vingapi vya kazi vilivyofikiwa au ni aina gani ya nyaraka ambazo wadukuzi wamezipata, lakini imesema katika barua iliyowaandikia wabunge kufichua jambo hilo na kwamba kwa sasa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa wahusika wameendelea kupata taarifa za Wizara ya Fedha.
Wizara inasema ilifahamu tatizo hilo Desemba 8 wakati mtoa huduma wa programu za watu wengine, BeyondTrust, aliporipoti kuwa wadukuzi waliiba ufunguo uliotumiwa na mkandarasi ambao uliisaidia kubatilisha mfumo na kufanikisha udukuzi kutokea mbali kwa vituo kadhaa vya kazi vya wafanyikazi wa wizara.
Forum