Takriban darzeni ya majimbo kutoka Kansas hadi New Jersey, yalikuwa katika tahadhari ya dhoruba ya theluji Jumapili mchana, kwa mujibu wa Idara ya Taifa Huduma za Hali ya Hewa, NWS, wakati maeneo kote kusini mwa Marekani yakikabiliwa na uwezekano wa dhoruba kubwa na hali ya baridi kali sana.
Zaidi ya watu milioni 60 kote Marekani wako katika aina fulani ya tahadhari ya hali ya hewa kulingana na shirika la habari la CNN, wakati mtandao wa kufuatilia usafiri wa anga FlightAware ukionyesha kufutwa kwa karibu safari 2,200 za ndege, huku nyingine zaidi ya 25,000 zikicheleweshwa.
Upepo mkali wa kasi kubwa kutokana na mfumo wa dhoruba, wa kwanza katika mwaka huu, umesababisha dhoruba kali huko Kansas na Missouri, wakati majimbo ya mashariki yakifunikwa na inchi kadhaa za theluji.
Gavana wa Kentucky Andy Beshear aliwaomba wakazi “kubaki nyumbani’ baada ya ajali kadhaa za gari kusababisha kufungwa kwa barabara kuu. Idara NWS imeonya pia kuhusu uwezekano wa kuanguka kwa miti kwenye sehemu nyingi, pamoja na kupotea kwa umeme.
Forum