Vera ameuomba Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mengine ya kimataifa yaingilie kati, baada ya kile alichokiita kuwa “jaribio la mauaji,’ dhidi ya Glas kwenye jela ya La Roca. "Shambulizi hilo ni matokeo ya serikali ambayo imemhukumu kwa hatari, mateso na kifo cha pole pole," Vera amesema katika mtandao wa kijamii wa X.
“Kuondolewa kwake kwa dharura kunathibitisha kile ambacho umekishutumu kila mara: kwa makusudi wanacheza na maisha yake,” Vera liasema. “Kama chochote kitamtokea, basi utakuwa uhalifu wa serikali. Idara ya magereza ya Ecuador SNAI, haijajibu obi la kutoa maoni.
Glas alikamatwa Aprili baada ya vikosi vya usalama vya Ecuador kuuvamia ubalozi wa Mexico mjini Quito, ambako alikuwa anakaa baada ya kuomba hifadhi. Wafuasi wake wanasema kwamba kukamatwa kwake kuna ushawishi wa kisiasa.
Makamu huyo wa rais wa zamani amehukumiwa kwa rushwa katika kesi nyingine mbili. Glas pia anakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya fedha zilizokusanywa kwa ajili ya ukarabati wa jimbo la pwani la Manabi, kufuatia tetemeko baya la ardhi la 2016.
Forum