Miili ya watu ilitapakaa mitaani, huku milio ya risasi ikisikika, na hospitali zikizidiwa nguvu katika mji mkubwa zaidi wa mashariki mwa Kongo siku ya Jumanne, huku waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, wakikabiliwa na upinzani kutoka kwa jeshi, na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.