Sudan Kusini inapanga kuanza tena uchimbaji mafuta ghafi baada ya mapigano yanayoendelea katika nchi jirani ya Sudan kusababisha uharibifu kwenye bomba la kusafirisha mafuta mapema mwaka huu.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema leo Jumanne kwamba imetoa taarifa muhimu na utafiti wa hivi karibuni kuhusu virusi vya Corona kwa jamuiya ya kimataifa na kwamba kazi ya kutafuta chanzo cha mlipuko wa virusi hivyo unastahili kufanyika katika nchi nyingine.
Waziri mkuu wa Ufaransa Francois Bayrou ameahidi msaada zaidi kwa watu wa kisiwa cha Mayitte, akiwa katika ziara hii leo kwenye kisiwa hicho katika Bahari hindi ambapo ameahidi ujenzi mpya, kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Chido.
Wanajeshi 23 wanakabiliwa na hukumu ya kifo au kifungo cha kati ya miaka 10 hadi 20 gerezani, baada ya kufikishwa mahakamani jana Jumatatu kwa mashtaka ya kunajisi, kuhepa kazi na makosa mengine jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Mahakama nchini Korea kusini imeidhinisha hati ya kukamatwa rais Yoon Suk Yeol, ambaye bunge lilipiga kura ya kumuondoa madarakani.
Miji mikuu kote duniani inajitayarisha kwa sherehe za mwaka mpya baada ya kuaga mwaka 2024 uliogubikwa na vita na msukosuko wa kisiasa.
Maafisa wa Russia wamesema leo jumanne kwamba mabaki ya ndege isiyokuwa na rubani iliyoharibiwa, yameangukia vitalu vya mafuta katika mji wa Smolensk na kusababisha moto.
Ukraine na Russia, zimefanya mabadilishano mapya ya wafungwa wa kivita Jumatatu, huku pande hizo mbili zikiwarejesha nyumbani jumla ya wafungwa zaidi ya 300 wa zamani.
Wadukuzi wa Kichina walifikia sehemu kadhaa za kazi za Wizara ya Fedha ya Marekani, na taarifa za siri baada ya kufanikiwa udukuzi kwa kutumia kampuni iliyopewa kandarasi ya kompyuta, wizara hiyo imesema Jumatatu.
Gavana wa Odesa, Oleh Kiper alisema kupitia mtandao wa Telegram vifusi vya Drone viliharibu majengo matano ya makazi.
Haya yanajiri mwaka mmoja baada ya serikali ya Sudan kusitisha uhusiano na jumuiya hiyo ya kikanda na kusitisha uanachama wake
Polisi nchini Kenya Jumatatu wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kulalamikia visa vya utekaji nyara vya wale wanaoonekana kuipinga serikali.
Pandisha zaidi