Vitisho dhidi ya Israel kutoka Syria bado vipo licha ya kauli za msimamo wa wastani za viongozi wa waasi waliomuondoa madarakani Rais Bashar al-Assad wiki moja iliyopita, waziri wa ulinzi wa Israel Katz alisema Jumapili, huku kukiwa na harakati za kijeshi za nchi yake kukabiliana na vitisho hivyo.
Viongozi kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS walikutana Jumapili katika mkutano kuhusu usalama na kuondoka kwenye jumuiya hiyo kwa serikali tatu zinazoongozwa na wanajeshi.
Raia watatu wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulizi la ndege isiyo kuwa na rubani lililofanywa na wanamgambo katika mji wa magharibi mwa Sudan wa El-Fasher huko Darfur Kaskazini, maafisa wamesema Jumapili.
Mazungumzo kati ya viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kumaliza mzozo wa mashariki mwa DRC hayakufanyika tena leo Jumapili kama ilivyotarajiwa kutokana na mivutano kati ya serikali za nchi hizo mbili, maafisa wamesema.
Wanajeshi wa Marekani wameanza kuondoka kidogo kidogo kutoka Okinawa hadi Guam, miaka 12 baada ya Japan na Marekani kukubaliana kuhusu marekebisho yao ili kupunguza mzigo mkubwa wa kuwepo kwa wanajeshi wa Marekani katika kisiwa cha kusini mwa Japan.
Vifaru wanne weupe wamekufa nchini Zimbabwe baada ya kunywa maji kutoka katika ziwa lililochafuliwa na maji taka ambalo pia ndilo msambazaji mkuu wa maji karibu na mji mkuu
Mazungumzo ya Umoja wa Mataifa yanayosimamiwa na Saudi Arabia yalishindwa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabiliana na ukame
Mchezaji soka wa zamani Mikheil Kave-lashvili amechaguliwa kuwa rais wa Georgia
Bunge la Korea Kusini limepiga kura kumshtaki kutaka kumuondoa madarakani Rais Yoon Suk Yeol kwa tangazo lake la muda mfupi la sheria ya kijeshi mwezi huu.
Rais mteule wa Ghana John Dramani Mahama amesema hataachana na mpango wa dola bilioni 3 wa kuokoa uchumi wa nchi hiyo na Shirika la Kimataifa la Fedha -IMF,
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Ijumaa amemteua waziri mkuu mpya Francois Bayrou, kiongozi wa chama cha mrengo wa kati baada ya mazungumzo magumu ili kumpata mrithi wa Michel Barnier aliyeondolewa na bunge wiki iliyopita, Ikulu ya Ufaransa imetangaza.
Niger Alhamisi ilitangaza kwamba imesitisha matangazo ya radio BBC kwa miezi mitatu, huku shirika hilo la utangazaji la Uingereza likiingia kwenye orodha ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vilivyoadhibiwa na serikali za kijeshi katika kanda ya Sahel.
Pandisha zaidi