Maelfu ya watu waliandamana Jumamosi katika mji mkuu wa Uturuki Ankara kuomba nyongeza ya kima cha chini cha mshahara, huku wakiimba nyimbo za kuitaka serikali kujiuzulu wakipeperusha bendera za upinzani na taifa.
Rais wa Russia Vladimir Putin Jumamosi amemuomba radhi rais wa Azerbaijan “kwa ajali hiyo mbaya” iliyotokea katika anga ya Russia ambapo ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan ilianguka baada ya mifumo ya ulinzi wa anga kutumiwa dhidi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Shambulizi la jeshi la Israel lililolenga wanamgambo wa Hamas limesababisha kufungwa kwa hospitali kuu huko kaskazini mwa Gaza na kushikiliwa kwa mkurugenzi wake, shirika la afya duniani na maafisa wa afya wamesema Jumamosi.
Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kukomesha vitendo vya utekaji nyara ambavyo vimeongezeka siku za hivi karibuni na kulaaniwa na makundi ya kutetea haki za binadamu, wanasheria na wanasiasa.
Ufaransa imekabidhi kambi yake ya kwanza ya kijeshi kama sehemu ya kujiondoa kijeshi kutoka Chad, majeshi ya Ufaransa na Chad yamesema Alhamisi.
Saa chache baadaye Wa-houthi walifyatua kombora katika uwanja wa ndege Ben Gurion na walirusha Drone kwenye mji wa Tel Aviv
Pyongyang imepeleka maelfu ya wanajeshi kuimarisha jeshi la Russia, ikijumuisha kwenye mkoa wa mpakani wa Kursk
Bunge lilipiga kura kutokua na imani na Scholz Desemba 16 baada ya serikali ya mseto ambayo ilisambaratika Novemba 6.
Rais wa Eritrea Asaias Afwerki, na mwenzake wa Somalia Sheikh Mohamud, Jumatano wamefanya mazunguzo ya kina yakiangazia ushirikiano pamoja na masuala ya kieneo yanayohusu mataifa yao.
Takriban watu 125 wameuawa nchini Msumbiji katika kipindi cha siku tatu za ghasia nchi nzima wakati wa maandamano yaliyoongozwa na upinzani dhidi ya matokeo ya uchaguzi, shirika lislo la kiserikali limesema siku ya Alhamis.
Wakaazi wa mji mkuu wa Syria wa Damascus wametoa wito wa kuwa na umoja baada ya ghasia kuzuka katika miji ya Tartous na Homs na shambulizi dhidi ya maofisa wa polisi lililosababisha vifo vya baadhi yao na kujeruhi wengine.
Pandisha zaidi