Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 06:04

Marais wa Eritrea na Ethiopia wakutana ili kujadili ushirikiano


Rais wa Eritrea Asaias Afwerki.
Rais wa Eritrea Asaias Afwerki.

Rais wa Eritrea Asaias Afwerki, na mwenzake wa Somalia Sheikh Mohamud, Jumatano wamefanya mazunguzo ya kina yakiangazia ushirikiano pamoja na masuala ya kieneo yanayohusu mataifa yao.

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya kigeni ya Eritrea imesema kuwa viongozi hao walisisitiza umuhimu wa Somalia kwenye udhibiti wa kieneo. Oktoba mwaka huu viongozi wa Misri, Eritrea na Somalia walikutana kwenye kongamano la siku tatu mjini Asmara, wakati hali ya taharuki ikiwa imetanda kwenye pembe ya Afrika, hasa kati ya Somalia na Ethiopia.

Mwanadiplomasia wa Somalia ambaye hakutaka kutajwa, aliambia VOA kwamba viongozi wote wawili Desemba 11 walizungumzia makubaliano ya Ankara kati ya Ethiopia na Somalia, yakilenga kumaliza taharuki ya kieneo. Kulingana na wizara ya mambo ya kigeni ya Eritrea, kwenye mazungumzo ya Jumatano rais wa Eritrea alisema kwamba ni muhimu kwa kanda hiyo kujiepusha na uingiliaji wa kigeni ambao mara nyingi hupelekea ghasia, akisisitiza umuhimu wa kutatua masuala kieneo.

Forum

XS
SM
MD
LG