Jeshi la Israel limeripoti kuwa lilifanya mashambulizi ya anga leo Ijumaa yakilenga miundombinu katika mpaka wa Syria na Lebanon karibu na kijiji cha Janta ambacho ilisema kilitumika kusafirisha silaha kwenda kwa kundi la Hezbollah.
Mapema leo jeshi la anga la Israeli-IAF lilipiga miundombinu ambayo ilitumika kusafirisha kimagendo silaha kupitia Syria hadi kwa kundi la kigaidi la Hezbollah nchini Lebanon katika kituo cha Janta kwenye mpaka wa Syria na Lebanon, jeshi limesema katika taarifa.
Haikueleza iwapo mashambulizi hayo yalikuwa upande wa Syria au Lebanon, lakini yamefanyika siku moja baada ya jeshi la Lebanon kuishutumu Israel kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kwa kushambulia ndani ya mipaka ya Lebanon na kuharibu miji Pamoja na vijiji vya kusini.
Hakuna kituo rasmi cha kukatisha karibu na Janta lakini eneo hilo linajulikana kwa harakati za kinyume cha sheria. Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon, UNIFIL pia kimeelezea wasiwasi wake juu ya uharibifu unaoendelea ambao unasababishwa na vikosi vya Israel huko kusini mwa Lebanon.
Forum