Ufaransa imekabidhi kambi yake ya kwanza ya kijeshi kama sehemu ya kujiondoa kijeshi kutoka Chad, majeshi ya Ufaransa na Chad yamesema Alhamisi.
Saa chache baadaye Wa-houthi walifyatua kombora katika uwanja wa ndege Ben Gurion na walirusha Drone kwenye mji wa Tel Aviv
Pyongyang imepeleka maelfu ya wanajeshi kuimarisha jeshi la Russia, ikijumuisha kwenye mkoa wa mpakani wa Kursk
Bunge lilipiga kura kutokua na imani na Scholz Desemba 16 baada ya serikali ya mseto ambayo ilisambaratika Novemba 6.
Rais wa Eritrea Asaias Afwerki, na mwenzake wa Somalia Sheikh Mohamud, Jumatano wamefanya mazunguzo ya kina yakiangazia ushirikiano pamoja na masuala ya kieneo yanayohusu mataifa yao.
Takriban watu 125 wameuawa nchini Msumbiji katika kipindi cha siku tatu za ghasia nchi nzima wakati wa maandamano yaliyoongozwa na upinzani dhidi ya matokeo ya uchaguzi, shirika lislo la kiserikali limesema siku ya Alhamis.
Wakaazi wa mji mkuu wa Syria wa Damascus wametoa wito wa kuwa na umoja baada ya ghasia kuzuka katika miji ya Tartous na Homs na shambulizi dhidi ya maofisa wa polisi lililosababisha vifo vya baadhi yao na kujeruhi wengine.
Viongozi wapya wa Syria Alhamisi walianzisha operesheni dhidi ya wanamgambo wenye uhusiano na rais aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad, kulingana na shirika la habari la serikali SANA.
Wahamiaji zaidi ya 10,000 walifariki dunia au kupotea mwaka 2024 wakati wakijaribu kufika Uhispania kwa njia ya bahari, shirika lisilo la kiserikali limesema Alhamisi, idadi hiyo ikiwa imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka uliopita na kubwa zaidi tangu mwaka 2007.
Madaktari wa Palestina wamesema shambulizi la Israel mapema Alhamisi limewaua wanahabari watano katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Gaza.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis Jumatano katika hotuba yake ya kawaida wakati wa Krismasi amewasihi “watu wa mataifa yote” kuwa na ujasiri katika mwaka huu Mtakatifu, kwa kuzima milio ya silaha na kumaliza migawanyiko inayoikumba Mashariki ya Kati, Ukraine, Afrika na Asia.
Pandisha zaidi