Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 12:51

Viongozi wapya wa Syria washambulia wapiganaji wanaomuunga mkono Assad


Kiongozi mpya wa Syria Ahmed al-Sharaa akikutana na viongozi wa vyama vya zamani vya waasi, Desemba 24, 2024.
Kiongozi mpya wa Syria Ahmed al-Sharaa akikutana na viongozi wa vyama vya zamani vya waasi, Desemba 24, 2024.

Viongozi wapya wa Syria Alhamisi walianzisha operesheni dhidi ya wanamgambo wenye uhusiano na rais aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad, kulingana na shirika la habari la serikali SANA.

Ripoti zimesema operesheni hiyo ililenga zaidi mkoa wa magharibi wa Tartous, na kwamba baadhi ya wanamgambo waliuawa.

Hayo yanajiri siku moja baada ya wapiganaji wanaomuunga mkono Assad kuua wapiganaji 14 wa kundi la waasi ambalo liliongoza mashambulizi yaliyopelekea kuondolewa madarakani kwa Assad.

Waziri mpya wa Mambo ya Ndani wa Syria aliandika kwenye mtandao wa Telegram kwamba watu 10 walijeruhiwa katika kile amekitaja kuwa “shambulio la kuvizuia”, na ameapa kukabiliana na yeyote atakayedhoofisha usalama wa Syria.

Forum

XS
SM
MD
LG