Waasi wa Yemen wamedai kufanya shambulizi kwenye mji wa biashara wa Tel Aviv nchini Israel leo Ijumaa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel kushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sanaa unaoshikiliwa na waasi na maeneo mengine nchini Yemen.
Mashambulizi hayo ya Israel siku ya Alhamisi yamefanyika wakati mkuu wa shirika la afya duniani-WHO anasema yeye na timu yake wanajiandaa kuondoka kutoka mji mkuu wa Yemen unaodhibitiwa na waasi wa ki-Houthi.
Saa chache baadaye leo Ijumaa Wa-houthi walisema walifyatua kombora katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion na walirusha ndege zisizo na rubani kwenye mji wa Tel Aviv pamoja na meli katika bahari ya Arabia.
Hakuna maelezo zaidi yaliyopatikana mara moja. Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Yemen imesema uwanja huo umepangwa kufunguliwa tena Ijumaa baada ya mashambulizi ambayo ilisema yalitokea wakati ndege za Umoja wa Mataifa zilikuwa zikijiandaa kwa safari yake kama iliyopangwa.
Forum