Takriban watu 125 wameuawa nchini Msumbiji katika kipindi cha siku tatu za ghasia nchi nzima wakati wa maandamano yaliyoongozwa na upinzani dhidi ya matokeo ya uchaguzi, shirika lislo la kiserikali limesema siku ya Alhamis.
Wakaazi wa mji mkuu wa Syria wa Damascus wametoa wito wa kuwa na umoja baada ya ghasia kuzuka katika miji ya Tartous na Homs na shambulizi dhidi ya maofisa wa polisi lililosababisha vifo vya baadhi yao na kujeruhi wengine.
Viongozi wapya wa Syria Alhamisi walianzisha operesheni dhidi ya wanamgambo wenye uhusiano na rais aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad, kulingana na shirika la habari la serikali SANA.
Wahamiaji zaidi ya 10,000 walifariki dunia au kupotea mwaka 2024 wakati wakijaribu kufika Uhispania kwa njia ya bahari, shirika lisilo la kiserikali limesema Alhamisi, idadi hiyo ikiwa imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka uliopita na kubwa zaidi tangu mwaka 2007.
Madaktari wa Palestina wamesema shambulizi la Israel mapema Alhamisi limewaua wanahabari watano katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Gaza.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis Jumatano katika hotuba yake ya kawaida wakati wa Krismasi amewasihi “watu wa mataifa yote” kuwa na ujasiri katika mwaka huu Mtakatifu, kwa kuzima milio ya silaha na kumaliza migawanyiko inayoikumba Mashariki ya Kati, Ukraine, Afrika na Asia.
Watu 21 wameuawa katika maandamano nchini Msumbiji, tangu mahakama ya juu ilipoidhinisha ushindi wa chama cha Frelimo siku ya Jumatatu.
Mashambulizi ya jeshi la Pakistan katika jimbo la Paktika, kusini mashariki mwa Afghanistan, yameua watu 46, wengi wao wakiwa watoto na wanawake.
Tetemeko la ardhi limesababisha maporomoko ya ardhi na uharibifu mkubwa kwenye miundo mbinu katika mji mkuu wa Port Villa, Vanuatu.
Uchunguzi wa awali unasema kwamba ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan iliyoanguka na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30, ilitokana na ndege hiyo kugonga ndege mnyama.
Walinzi wa pwani ya Uhispania wamewaokoa darzeni ya wahamiaji kutoka visiwa vya Canary leo Jumatano.
Watoto 27 wamezaliwa hospitali nchini Kenya siku ya Krismas. Kati ya watoto hao, kumi ni wa kiume na 17 ni wa kike. Watoto hao walizaliwa na wanawake walio kati ya umri wa miaka 16 hadi 37.
Pandisha zaidi