Wizara ya afya ya Lebanon ilisema shambulizi la Israel Jumatatu lilimuuwa mtu mmoja kusini mwa Lebanon, huku jeshi la Lebanon likisema shambulio la Israel lilimjeruhi mwanajeshi katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Rais wa Chad Mahamat Deby alisema uamuzi wa kusitisha mkataba wa kijeshi wa nchi hiyo na Ufaransa umechukuliwa kwa sababu umepitwa na wakati katika matamshi yake ya kwanza hadharani tangu kutangazwa kwa mshangao wiki iliyopita.
Uamuzi wa kutatanisha wa refa katika mechi ya mpira wa miguu ulizua vurugu na mkanyagano katika mechi moja ya soka kusini mashariki mwa Guinea, na kuuwa watu 56 kulingana na idadi ya awali, serikali ilisema Jumatatu.
Ziara ya Rais Joe Biden nchini Angola – ni ya kwanza kufanywa na Rais wa Marekani katika taifa hilo la kusini magharibi mwa Afrika – ziara hiyo inahusu zaidi ujenzi wa njia ya reli ambayo itasafirisha madini yenye thamani kutoka Katikati mwa bara hilo kupitia bandari ya Angola.
Rais wa Marekani, Joe Biden, Jumapili, alifanya kumbukumbu ya UKIMWI, katika bustani ya kusini mwa White House kwa mara ya kwanza, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.
Mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa itaanza kusikiliza kesi kubwa zaidi katika historia Jumatatu, na kuchukuwa wiki mbili kuhusiana na mataifa duniani yanayotakiwa kukabiliana mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia mataifa yaliyo hatarini kukabiliana na hali hiyo.
Mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini Namibia, Panduleni Itula, Jumamosi alisema kwamba chama chake hakitatambua matokeo ya uchaguzi wa rais wenye utata uliogubikwa na vurugu na madai ya wizi wa kura.
Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kushughulikia mzozo wa Sudan unaozidi kuwa mbaya, akisisitiza mateso kwa mamilioni ya watu waliokoseshwa makazi kutokana na mzozo huo.
Rais wa Kenya Dr. William Ruto, amesema kwamba ni jukumu la pamoja la viongozi wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha kwamba kanda nzima ina usalama na utulivu.
Waasi nchini Syria wamedhibiti sehemu kubwa ya mji wa Aleppo ambao ndio mji mkubwa zaidi nchini Syria.
Hesabu ya kura inaendelea nchini Iceland katika uchaguzi wa bunge uliofanyika leo Jumamosi, baada ya kutokea hali ya kutoelewana kuhusu maswala ya uhamiaji, sera ya nshati na uchumi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kwamba hatua ya nchi hiyo kuruhusiwa kuwa mwanachama wa NATO inaweza kumaliza kile amekitaja kama hatua moto ya vita vya Russia.
Pandisha zaidi