Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:38

Waasi waudhibithi mji mkuu wa Aleppo, Syria


Waasi wakipiga doria katikati mwa mji wa Aleppo. Nov. 30, 2024.
Waasi wakipiga doria katikati mwa mji wa Aleppo. Nov. 30, 2024.

Waasi nchini Syria wamedhibiti sehemu kubwa ya mji wa Aleppo ambao ndio mji mkubwa zaidi nchini Syria.

Hii ni mara ya kwanza kwa waasi kuudhibithi mji huo tangu mwaka 2016.

Mapigano yanaendelea kati ya waasi na wanajeshi wa serikali, huku ndege za kivita za Syria zikitekeleza mashambulizi katika mji huo.

Shirika la kufuatilia haki za binadamu nchini Syria limesema kwamba kundi la wapiganaji la Hayat Tahir al-Sham, linaloongozwa na tawi la Al-Qaeda nchini Syria, kwa ushirikiano na makundi mengine ndani, limedhibiti sehemu kubwa ya Aleppo, vituo vya serikali na magereza.

Shirika hilo limesema kwamba Gavana wa Aleppo na uongozi wa polisi na maafisa wa usalama wameondoka Aleppo, huku wanajeshi wa serikali wakikimbilia huko Al-Safirah.

Shirika la habari la Reuters, limeripoti kwamba serikali ya rais Bashar Al-Assad imefunga uwanja wa ndege wa Aleppo na Barabara zote kuingia mjini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG