Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo limepoteza eneo Jumatatu katika mapigano na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa nchi, duru za kijeshi na za ndani zinasema, siku moja baada ya mkutano wa amani kati ya marais wa nchi hizo mbili kufutwa.
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wanapigana na kufa pamoja na vikosi vya Russia, katika vita vya Moscow dhidi ya Ukraine, kwa mujibu wa tathmini ya karibuni kutoka Pentagon.
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, Jumatatu amelilaumu jeshi la nchi, akidai linaficha kuhusu ndege zisizo na rubani zisizo na taarifa kamili zinazoruka usiku mashariki mwa Marekani, hata hivyo Pentagon ilikanusha mara moja madai yake.
Umoja wa Ulaya Jumatatu kwa mara ya kwanza uliweka vikwazo vyenye mamlaka kamili, ikiwa ni pamoja na kuzuia mali na marufuku ya viza, kwa makampuni ya Kichina kwa kuipatia Russia vifaa vya kijeshi, kwa vita dhidi ya Ukraine.
Mahakama itafanya kikao cha kwanza cha umma Disemba 27 baada ya majaji sita wa mahakama kukutana.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ataitembelea Ethiopia na Somalia mapema mwaka ujao baada ya kufanya makubaliano ya kumaliza mivutano kati ya majirani hao wa Pembe ya Afrika, amesema Jumapili kupitia mtandao wa X.
Ubalozi wa Qatar, nchini Syria, utaanza tena shughuli zake Jumanne, ufalme wa Ghuba ulitangaza Jumapili wakati wanadiplomasia wake walipoitembelea nchi hiyo na kukutana na serikali yake ya mpito kufuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Bashar al-Assad.
Umoja wa Mataifa utaitisha kamati ya ufundi ya wataalamu wa Libya kutatua masuala mazito na kuiweka nchi hiyo kwenye mwelekeo wa uchaguzi wa kitaifa unaosubiriwa kwa muda mrefu, kaimu mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) amesema Jumapili.
Kiwanda kimoja cha kusafisha mafuta cha Libya kilichopo magharibi mwa Libya kimefungwa baada ya mapigano kati ya makundi yenye silaha kuzuka mapema Jumapili na kusababisha moto kwenye miundombinu, kampuni ya mafuta ya serikali NOC imesema.
Kimbunga kilichopewa jina la Chido kimetua kaskazini mwa Msumbiji baada ya kusababisha hasara kubwa kwenye kiswa cha Mayotte.
Vitisho dhidi ya Israel kutoka Syria bado vipo licha ya kauli za msimamo wa wastani za viongozi wa waasi waliomuondoa madarakani Rais Bashar al-Assad wiki moja iliyopita, waziri wa ulinzi wa Israel Katz alisema Jumapili, huku kukiwa na harakati za kijeshi za nchi yake kukabiliana na vitisho hivyo.
Viongozi kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS walikutana Jumapili katika mkutano kuhusu usalama na kuondoka kwenye jumuiya hiyo kwa serikali tatu zinazoongozwa na wanajeshi.
Pandisha zaidi