Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 16, 2024 Local time: 11:42

Rais wa Uturuki kutembelea Ethiopia na Somalia


Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan, akiwa na Rais wa Somalia, Hasan Sheek Mohamud, na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, baada ya mkutano wao na wanahabari, mjini Ankara, Uturuki, Desemba 11, 2024.
Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan, akiwa na Rais wa Somalia, Hasan Sheek Mohamud, na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, baada ya mkutano wao na wanahabari, mjini Ankara, Uturuki, Desemba 11, 2024.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ataitembelea Ethiopia na Somalia mapema mwaka ujao baada ya kufanya makubaliano ya kumaliza mivutano kati ya majirani hao wa Pembe ya Afrika, amesema Jumapili kupitia mtandao wa X.

“Nitazitembelea Ethiopia na Somalia katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka mpya,” aliandika katika ujumbe akigusia makubaliano kati ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud mjini Ankara, Desemba 11.

Wawili hao walikubali kumaliza mzozo wao wa karibu mwaka mzima baada ya saa kadhaa za mazungumzo yaliyosimamiwa na Erdogan, ambaye alisifu mafanikio hayo kuwa ni historia.

Mzozo huo ulianza Januari wakati Ethiopia isiyo na bandari ilipofikia makubaliano na mkoa uliojitenga nchini Somalia wa Somaliland kukodisha sehemu ya ufukwe kwa ajili ya bandari na kambi ya kijeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG