Tume ya uchaguzi nchini Chad imeliomba jeshi la taifa kusaidia kuwalinda maafisa wa uchaguzi na wagombea kuelekea uchaguzi wabunge na serikali za mitaa hapo Desemba 29.
Sehemu za kisiwa cha Mayotte kilicho chini ya usimamizi wa Ufaransa, zinaendelea kukadiria hasara kubwa leo Jumatano, baada ya kimbunga Chido kupiga kisiwa hicho jumamosi.
Kiongozi wa muungano wa kitaifa wa Syria Hadi al-Bahra, waliomuondoa rais Bashar Al-Assad amesema kwamba serikali ya mpito ya Syria inastahili kuhusisha kila chama cha Syria na wala sio kuwa na ubaguzi.
Mahakama ya juu nchini Ghana imetupilia mbali kesi mbili tofauti zilizokuwa zimewasilishwa kama rufaa kupinga mojawapo ya sheria kandamizi zaidi dhidi ya watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.
Mahakama ya juu nchini Ghana Jumatano imetupilia mbali rufaa mbili za kubatilisha kifungu cha sheria kilichokuwa kimepingwa kwamba kinakandamiza vikali haki za wapenzi wa jinsia moja, sheria ambayo ilipitishwa na wabunge mapema mwaka huu.
Katika mji wa Goma, kundi la waandishi wa habari wa Congo wanakabiliana na habari potofu chungu nzima kuhusu afya na matibabu, ambazo ni hatari kubwa sana kwa umma.
Idadi ya vifo kutokana na kimbunga Chido nchini Msumbiji imeongezeka kutoka 11 hadi 45, idara ya taifa ya usimamizi wa majanga imesema Jumatano.
Madaktari Jumatano wamesema mashambulizi ya anga ya Israel yameua watu 12 katika Ukanda wa Gaza. Mashambulizi hayo ni pamoja na shambulizi lililofanyika katika mji wa Beit Lahiya, kaskazini mwa Gaza, ambalo liliua watu 10, madaktari wamesema.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Mkurugenzi Mtendaji wa bima ya afya ya UnitedHealthcare ameshtakiwa pia kwa mauaji kama kitendo cha kigaidi, waendesha mashtaka wamesema Jumanne wakiwa wanafanya kazi kumfikisha katika mahakama ya New York kutoka Pennsylvania.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Jumanne ameonya vita bado havijakwisha, nchi hiyo ni tete na inakabiliwa na changamoto nyingi, lazima iende kwa kasi kuelekea kipindi cha mpito wa kisiasa kinacho jumuisha pande zote.
Ukraine Jumanne imedai imehusika na mauaji ya jenerali mwandamizi wa Russia, kwenye mitaa ya Moscow kwa mlipuko wa bomu uliofichwa kwenye jengo la makazi yake.
Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo limepoteza eneo Jumatatu katika mapigano na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa nchi, duru za kijeshi na za ndani zinasema, siku moja baada ya mkutano wa amani kati ya marais wa nchi hizo mbili kufutwa.
Pandisha zaidi