Netumbo Nandi-Ndaitwah amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais nchini Namibia.
Maafisa wa Palestina, Jumanne wamesema Fatah, na kundi la wanamgambo wa Hamas walifikia karibu kupata makubaliano ya mipango kuhusu Gaza baada ya vita.
Umoja wa Mataifa, Jumanne umesema maelfu ya Wasyria wamekoseshwa makazi kutokana na mapigano ya karibuni baina ya waasi na serikali kaskazini magharibi mwa Syria, wakati waasi wakiendelea kutwaa maeneo zaidi.
Serikali ya Ufaransa inakabiliwa na kura ya kutokuwa na imani Jumatano, hatua ambayo inaweza kuisumbua serikali ya waziri mkuu Michael Barnier.
China Jumanne imeieleza mahakama kubwa ya Umoja wa Mataifa kwamba mikataba ya sasa ya Umoja wa Mataifa inatoa misingi juu ya wajibu kisheria wa mataifa kukabiliana na kuongezeka kiwango cha joto, na athari za kuchangia kwao kwa muda mrefu tatizo hilo.
Rais Joe Biden wa Marekani ameanza ziara ya siku mbili nchini Angola kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Joao Lourenco, juu ya ushirikiano wa kibiashara na uchumi.
Zaidi ya watu 100 wanahofiwa kupotea na wengine 17 wamefariki baada ya maporomoko ya ardhi ya Jumatano kwenye Mlima Elgon
"Tutafanya Chuma cha Marekani kuwa na nguvu na bora kwa mara nyingine, na hili litafanyika haraka, nitazuia mpango huu kutokea".
Vitisho vya Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, vya kuweka ushuru vimeleta mvutano baina ya Mexico na Canada, baada ya maafisa wa Canada kusema matatizo ya mpaka wa mataifa hayo mawili hayapaswi kulinganishwa.
Mkuu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Jumatatu amesema kwamba watoto wanajumuisha takriban nusu ya wanachama wa makundi yenye silaha ya Haiti, na kutoa mwito wa kulindwa kwao.
Utawala wa Rais Biden, wa Marekani, Jumatatu umetangaza kuweka vikwazo kadhaa vipya kwa bidhaa kwenda China, vikizuia kuuzwa kwa vifaa muhimu vya teknolojia za viwandani, na vile vikubwa vya kuweka kumbukumbu za kompyuta.
Serekali ya visiwa vya Ugiriki vya Rhodes, na Lemnos, imetangaza hali ya dharura Jumatatu, baada ya dhoruba kukumba visiwa hivyo na kusababisha vifo vya watu wawili na kufanya uharibifu mkubwa.
Pandisha zaidi