Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 07:12

Raia wa Syria wakimbia makazi yao


Umoja wa Mataifa, Jumanne umesema maelfu ya Wasyria wamekoseshwa makazi  kutokana na mapigano ya karibuni baina ya waasi na serikali kaskazini magharibi mwa Syria, wakati waasi wakiendelea kutwaa maeneo zaidi.

Adam Abdelmoula, mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya misaada ya kibinadamu wa Syria, amewaambia wanahabari mjini Damascus, kwamba wakati maelfu ya watu wanawasili katikati na kusini mwa nchi, huku wengi wakikwama katika uwanja wa mapambano wakishindwa kufika maeneo salama ya nchi.

Amesema kwamba mapigano yaliyo ongezeka ya makombora na angani yamewakosesha makazi raia kutoka miji ua Idlin, Aleppo, na Hama.

Kumekuwa na ripoti za vifo vya raia, lakini msemaji huyo amesema hali kamili ilivyo bado haijajulikana. Kaskazini mwa Aleppo inakadiriwa watu 125,000 wanatarajia kuelekea upande wa mashariki.

Forum

XS
SM
MD
LG