Mamlaka za Ujerumani zilipokea taarifa za tahadhari mwaka jana kuhusu mshukiwa wa shambulizi la gari kwenye soko la Christmas, ofisi ya serikali imesema Jumapili, huku maelezo zaidi yakitolewa kuhusu watu watano waliouawa katika shambulizi hilo.
Kiongozi mpya wa Syria Ahmed al-Sharaa Jumapili amewambia viongozi wa jamii ya walio wachache nchini Lebanon ya Druze kwamba nchi yake haitoingilia kati kwa nia mbaya katika masuala ya Lebanon na kwamba itaheshimu uhuru wa jirani yake.
Polisi nchini Nigeria Jumapili wamesema idadi ya vifo katika matukio mawili ya mkanyagano nje ya vituo vya kugawa chakula kwa watu maskini imeongezeka hadi 32.
Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza usiku kucha hadi Jumapili yameua watu 20 wakiwemo watoto watano, maafisa wa idara za matibabu za Palestina wamesema.
Baraza la Seneti la Marekani mapema Jumamosi asubuhi limepitisha mswada wa bajeti kuifadhili serikali kuu ya Marekani hadi mwezi Machi mwakani.
Wajerumani Jumamosi wameomboleza waathirika wa shambulizi lililofanywa na daktari raia wa Saudi Arabia ambaye aliendesha kwa makusudi gari lake ndani ya umati wa watu na kuwagonga wale waliokuwa kwenye soko la kuuza bidhaa za siku kuu ya Christmas, na kuua watu watano.
Polisi wa Zambia wamesema wamewakamata watu wawili kwa madai ya kujaribu “kumdhuru” rais wa taifa hilo la kusini mwa Afrika kwa kutumia uchawi.
Watu 20 waliuawa Ijumaa katika mashambulizi kwenye vijiji kadhaa katikati mwa Mali, yanayodaiwa kutekelezwa na wanajihadi, vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo wamesema.
Ghana inakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara. Baadhi ya waandishi wa habari wana matumaini ya kukabiliana na hali hiyo kwa kutoa ripoti sahihi.
Vita vya Karibu miezi 20 nchini Sudan vimeiweka nchi hiyo katika hali ngumu sana, wakati baadhi ya maeneo yenye mahitaji mkubwa hayafikiwi kabisa ili kuweza kupata mahitaji ya kibinadamu
Shirika la afya duniani WHO na serikali ya Rwanda, wametangaza leo ijumaa kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg, wenye dalili kama Ebola.
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amemfuta kazi mkuu wa majeshi na maafisa wengine wa ngazi ya juu katika jeshi la taifa, katika mabadiliko makubwa ndani ya jeshi wakati mapigano makali yanaendelea kati ya jeshi la serikali na waasi mashariki mwa DRC.
Pandisha zaidi