Mkuu wa majeshi Jenerali Christan Tshiwewe, ambaye amekuwa ofisini tangu Oktoba 2022, amefutwa kazi na nafasi hiyo kuchukuliwa na Luteni Jenerali Jules Banza Mwilambwe.
Jeshi la DRC limekuwa likipigana dhidi ya zaidi ya makundi ya wapiganaji 100 kwa miaka kadhaa, mashariki mwa nchi hiyo kuliko na utajiri mkubwa wa madini.
Mapigano yamesababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu.
Zaidi ya watu milioni 7 wamekoseshwa makazi na mamia kuuawa mwaka huu.
Miongoni mwa makundi ya waasi yanayopigana na wanajeshi wa serikali ni M23 ambalo serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa wanasema wanaungwa mkono na serikali ya nchi Hirani ya Rwanda.
Forum