Syria haitoingilia kati kamwe kwa nia mbaya katika masuala ya Lebanon, inaheshimu uhuru wa Lebanon, umoja wa maeneo yake, uhuru wa maamuzi yake pamoja na usalama na utulivu wake,” Sharaa amewaambia viongozi wa jamii ya Druze Walid na Taymur Jumblatt.
Walid Jumblatt ni kiongozi wa kwanza wa Lebanon kukutana na Sharaa tangu kundi lake la Kiislamu Hayat Tahrir al-Sham na makundi ya waasi washirika wake kuanzisha mashambulizi mwezi uliopita, na kuuteka mji wa Damascus tarehe 8 Disemba na kumuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Bashar al-Assad.
Walid Jumblatt, mkosoaji mkubwa wa muda mrefu wa Assad na baba yake Hafez ambaye aliiongoza Syria kabla ya mwanawe, aliwasili Damascus Jumapili akiongoza ujumbe wa wabunge na viongozi wa kidini kutoka jami ya walio wachache nchini Lebanon ya Druze.
Forum