“Vijiji sita vya wilaya ya Bandiagara vilishambuliwa siku ya Ijumaa na wanajihadi. Ghala za kuhifadhi chakula zilichomwa moto, raia walikimbia, na watu 20 waliuawa,” afisa wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia AFP.
Chanzo cha usalama kimeithibitishia AFP leo Jumamosi kwamba vijiji vitano vya wilaya ya Bandiagara vilishambuliwa Ijumaa, na watu 21 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Forum