Kampuni kubwa ya bima yenye makao yake Uswizi Alhamisi imesema majanga kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha hasara ya kiuchumi ya dola bilioni 310 ulimwenguni mwaka 2024.
Israel Alhamisi imetupilia mbali ripoti ya shirika la haki za binadamu Amnesty International ambayo inaishtumu nchi hiyo kwa kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ikiitaja kuwa “uongo mtupu”.
Wabunge wa Ufaransa Jumatano wamepiga kura ya kuiondoa serikali ya waziri mkuu Michel Barnier baada ya miezi mitatu tu ikiwepo madarakani, katika hatua ya kihistoria ambayo inaiweka tena nchi hiyo katika hali tete ya kisiasa.
Baada ya miezi minne, pamoja na kufukuzwa kwa ujumbe wa serikali, mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yaliyokwama yameanza tena Jumatano nchini Kenya, ikiwa juhudi ya karibuni zaidi ya kumaliza ghasia ambazo zimevuruga kabisa uchumi na uthabiti wa taifa hilo changa.
Katika kusikilizwa kwa kesi Jumatano, ndani ya mahakama ya kimataifa ya haki ya The Hague, Marekani imejibu kwamba sheria za haki za binadamu za mataifa hazina mashiko kwa wajibu wa kisheria kwa mabadiliko ya hali ya hewa.
Israel ilifanya mashambulizi zaidi yakilenga Gaza Jumatano, ambapo maafisa wa Palestina wanaripoti dazeni ya vifo vimetokea na majeruhi.
Idara za serekali ya Marekani, zilifanya mkutano wa siri na Maseneta Jumatano, kuhusu udukuzi wa China ambao unajulikana kama “Salt Typhoon,” uliojikita ndani kabisa mwa mashirika ya mawasiliano ya simu ya Marekani, na kuiba taarifa za simu za Marekani.
Netumbo Nandi-Ndaitwah amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais nchini Namibia.
Maafisa wa Palestina, Jumanne wamesema Fatah, na kundi la wanamgambo wa Hamas walifikia karibu kupata makubaliano ya mipango kuhusu Gaza baada ya vita.
Umoja wa Mataifa, Jumanne umesema maelfu ya Wasyria wamekoseshwa makazi kutokana na mapigano ya karibuni baina ya waasi na serikali kaskazini magharibi mwa Syria, wakati waasi wakiendelea kutwaa maeneo zaidi.
Serikali ya Ufaransa inakabiliwa na kura ya kutokuwa na imani Jumatano, hatua ambayo inaweza kuisumbua serikali ya waziri mkuu Michael Barnier.
China Jumanne imeieleza mahakama kubwa ya Umoja wa Mataifa kwamba mikataba ya sasa ya Umoja wa Mataifa inatoa misingi juu ya wajibu kisheria wa mataifa kukabiliana na kuongezeka kiwango cha joto, na athari za kuchangia kwao kwa muda mrefu tatizo hilo.
Pandisha zaidi