Moja ya shambulizi la Israel limelenga hema lililotumiwa na watu waliokosa makazi na kuwauwa watu 21, na kujeruhi 28 kusini mwa Gaza, kwa mujibu wa Atif al-Hout mkurugenzi wa hopsitali ya Nasser, katika mji wa karibu wa Khan Younis.
Jeshi la Israel limesema ndege ilimlenga kiongozi wa juu wa wanamgambo wa Hamas, aliyehusika na shughuli za kigaidi katika eneo hilo.
Takriban maiti watano walipelekwa hospitalini, lakini imekuwa vigumu kupata idadi kamili ya waliofariki kwa sababu miili imekatika viungo, mingine haina vichwa ama kuungua.
Shambulizi lilipiga eneo la Muwasi, ambapo kuna kambi katika mwambao inayohifadhi maelfu ya watu waliokimbia makazi.
Maafisa wanasema kwingineko Gaza watu wanane wameuwawa wakiwemo watoto.
Forum