Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 13:04

Israel yatupilia mbali tuhuma za kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina


Nembo ya Amnesty International
Nembo ya Amnesty International

Israel Alhamisi imetupilia mbali ripoti ya shirika la haki za binadamu Amnesty International ambayo inaishtumu nchi hiyo kwa kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ikiitaja kuwa “uongo mtupu”.

“Shirika hilo lenye msimamo wa kuegemea kwa mara nyingine limetoa ripoti ya uzushi ambayo ni ya uongo mtupu yenye msingi wa uongo,” wizara ya mambo ya nje ya Israel ilisema katika taarifa.

Taarifa hiyo imesema badala yake shambulizi baya la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel ndilo lilikuwa “mauaji ya kimbari”.

Taarifa hiyo imesema “Israel inajihami na inafanya hivyo kwa mujibu wa sheria za kimataifa.”

Amnesty International imesema uchunguzi wake ulizingatia “taarifa za kudhalilisha utu na mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa na maafisa wa serikali na jeshi la Israel”, picha za satelaiti zilizoonyesha uharibifu, kazi ya uwanjani na ripoti za wakazi wa Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG