Baraza la Seneti la Marekani mapema Jumamosi asubuhi limepitisha mswada wa bajeti kuifadhili serikali kuu ya Marekani hadi mwezi Machi mwakani.
Wajerumani Jumamosi wameomboleza waathirika wa shambulizi lililofanywa na daktari raia wa Saudi Arabia ambaye aliendesha kwa makusudi gari lake ndani ya umati wa watu na kuwagonga wale waliokuwa kwenye soko la kuuza bidhaa za siku kuu ya Christmas, na kuua watu watano.
Polisi wa Zambia wamesema wamewakamata watu wawili kwa madai ya kujaribu “kumdhuru” rais wa taifa hilo la kusini mwa Afrika kwa kutumia uchawi.
Watu 20 waliuawa Ijumaa katika mashambulizi kwenye vijiji kadhaa katikati mwa Mali, yanayodaiwa kutekelezwa na wanajihadi, vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo wamesema.
Ghana inakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara. Baadhi ya waandishi wa habari wana matumaini ya kukabiliana na hali hiyo kwa kutoa ripoti sahihi.
Vita vya Karibu miezi 20 nchini Sudan vimeiweka nchi hiyo katika hali ngumu sana, wakati baadhi ya maeneo yenye mahitaji mkubwa hayafikiwi kabisa ili kuweza kupata mahitaji ya kibinadamu
Shirika la afya duniani WHO na serikali ya Rwanda, wametangaza leo ijumaa kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg, wenye dalili kama Ebola.
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amemfuta kazi mkuu wa majeshi na maafisa wengine wa ngazi ya juu katika jeshi la taifa, katika mabadiliko makubwa ndani ya jeshi wakati mapigano makali yanaendelea kati ya jeshi la serikali na waasi mashariki mwa DRC.
Wanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani kutoka utawala wa Joe Biden wako Damascus, Syria kwa mkutano na maafisa wa utawala wa Syria wakiongozwa na Hayat Tahrir al-Sham.
Mswada wa kufadhili bajeti ya serikali kuu unaoungwa mkono na rais mteule Donald Trump, umeshindwa kupitishwa na baraza la wawakilishi.
Bilionea Elon Musk, anatarajiwa kujiunga na utawala wa rais mteule wa Marekani Donald Trump katika kuzungumzia uchaguzi wa Ujerumani, ambapo ameutaja mrengo wa kulia kuwa utawala mbadala kwa nchi hiyo.
Russia imemhukumu mkazii wa mkoa wa Lugansk, mashariki mwa Ukraine, kifungo cha miaka 16 gerezani kwa ‘uhaini wa hali ya juu’.
Pandisha zaidi