Mrengo wa kulia wa Ujerumani unashikilia nafasi ya pili katika ukusanyaji maoni na huenda ukapata idadi kubwa ya viti katika uchaguzi huo.
Hata hivyo, mashirika yenye ushawishi nchini Ujerumani yameapa kutowaunga mkono wanasiasa wa mrengo wa kulia.
Ujerumani, ambayo ndio nchi yenye nguvu zaidi Ulaya, inatarajiwa kuandaa uchaguzi Februari 23 baada ya utawala wa mrengo wa kati unaoongozwa na kansela Olaf Scholz, kuanguka.
Musk, ambaye ndiye tajiri mkubwa duniani, anaunga mkono vyama vyenye msimamo mkali dhidi ya uhamiaji kote ulaya.
Forum