Raia wa Msumbiji Jasten Mabulesse Candunde, mwenye umri wa miaka 42, na mkuu wa kijiji cha Zambia Leonard Phiri, mwenye umri wa miaka 43, walikamatwa katika mji mkuu Lusaka, ilisema taarifa ya polisi iliyotolewa Ijumaa.
“Washukiwa wamekutwa na hirizi za aina mbalimbali ikiwemo kinyonga hai na wanadaiwa kuwa wachawi,” taarifa ya polisi imesema.
“Inasemekana kuwa walikuwa wanakusudia kutumia hirizi kumdhuru Rais Hakainde Hichilema.”
Polisi wamedai wawili hao waliajiriwa na kaka wa mbunge wa upinzani anayekabiliwa na kesi ya wizi, jaribio la mauaji na kutoroka jela.
Wanakabiliwa na mashtaka ya ukatili wa wanyama na watafikishwa mahakamani hivi karibuni, imesema taarifa ya polisi.
Forum