Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 20:10

Russia imehukumu raia wa Ukraine kwa uhaini


Rais wa Russia Vladmir Putin Dec 19, 2024
Rais wa Russia Vladmir Putin Dec 19, 2024

Russia imemhukumu mkazii wa mkoa wa Lugansk, mashariki mwa Ukraine, kifungo cha miaka 16 gerezani kwa ‘uhaini wa hali ya juu’.

Hayo ni kulingana na maafisa wa usalama wa Moscow.

Kila mara, Moscow kuwapa adhabu kali watu kutokana na mashtaka wanayoshutumiwa kwa kuifanyia upelelezi Ukraine na imekuwa ikiwafunga gerezani raia wa Ukraine ndani ya Russia na katika mikoa wanayoikalia kimabavu.

Hukumu hiyo imejiri wakati rais wa Russia Vladimir Putin ametoa wito kwa idara ya a usalama kuchukua hatua kali dhidi ya ugaidi, wakati vita vya Russia dhidi ya Ukraine vikiwa vinaendelea kwa karibu mwaka wa tatu.

Mwanamme huyo amabye jina lake halijatajwa, amehukumiwa leo Ijumaa katika mahakama ya kijeshi, katika mji wa Rostov-on-Don, kusini mwa Russia.

Wakati huo huo maafisa wanasema shambulizi la kombora la masafa marefu lililotekelezwa na Russia dhidi ya mji mkuu wa Kyiv nchini Ukraine, limemuua mtu mmoja na kujeruhi wengine tisa.

Moscow imedai kwamba imejibu shambulizi la Ukraine dhidi ya Russia, lililotekelezwa kwa kutumia silaha zilizotengenezwa nchini Marekani.

Milipuko mitatu imesikika mjini Kyiv, muda mfupi kabla ya asubuhi leo ijumaa.

Jeshi la anga la Ukraine limesema limenasa makombora Matano ya masafa marefu yaliyorushwa na Russia kuelekea Kyiv.

Maafisa wamesema mabaki ya makombora hayo yaliyokuwa yanaanguka yamesababisha uharibifu na moto katika wilaya tatu.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema mashambulizi hayo yalikuwa ya kujibu makombora ya Ukraine dhidi ya Russia katika mpaka wa Rostov, siku mbili zilizopita.

Forum

XS
SM
MD
LG