Watoto 27 wamezaliwa hospitali nchini Kenya siku ya Krismas. Kati ya watoto hao, kumi ni wa kiume na 17 ni wa kike. Watoto hao walizaliwa na wanawake walio kati ya umri wa miaka 16 hadi 37.
Mahakama moja ya Amsterdam nchini Uholanzi Jumanne imewahukumu vifungo vya hadi miezi 6 jela wanaume watano kwa ghasia ambazo zilizuka kwenye michuano ya soka katika ligi ya UEFA Europa, wakati wa mechi kati ya timu ya Uholanzi ya Ajax na Maccabi Tel Aviv ya Israel hapo Novemba.
Baraza Kuu la Iran linaloshugulikia kulinda usalama wa mitandao limepiga kura Jumanne kuondoa marufuku kwenye jukwaa la mawasiliano ya WhatsApp, ambalo liliwekewa masharti kwa zaidi ya miaka miwili, shirika la habari la serikali limesema.
Utawala mpya wa Syria umesema kwamba makundi yenye silaha yamekubali kuachana na mapigano na kujiunga na jeshi la serikali.
Mji mtakatifu wa Bethlehem, kwenye Ukingo wa Magharibi hautakuwa na shamra shamra za krismasi kutokana na vita vya Gaza.
Mji mkuu wa Msumbiji, Maputo ulikuwa mtupu Jumanne, siku ya mkesha wa Krismasi, huku kukiwa na ulinzi mkali katika vituo muhimu vya mji huo, siku moja baada ya mahakama ya katiba kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa Oktoba.
Raia wa Cameroon watapiga kura mwaka ujao kumchagua rais kwa muhula mwingine wa miaka saba. Chaguzi za awali katika taifa hili la Afrika ya Kati zilikumbwa na taarifa potofu ambazo zilichochea machafuko kwenye mitandao ya kijamii.
Mamia ya wakristo wameandamana katika mji mkuu wa Syria, Damascus, baada ya mti wa krismasi kuchomwa moto katika wilaya ya al-Suqaylabiyah, mjini Hama, kaskazini mwa nchi hiyo.
Wachunguzi wa Umoja wa mataifa wamepata taarifa zaidi kuhusu mauaji ya halaiki ya watu yaliyotekelezwa na kundi la wahalifu la Wharf Jérémie mjini Port-au-Prince, Haiti, mapema mwezi huu.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan amesema kwamba wapiganaji wa kikurdi wa YPG nchini Syria, hawana nafasi tena nchini Uturuki.
Wanachama wa kamati ya maandalizi ya utawala wa rais mteule wa Marekani Donald Trump, wanapanga mikakati ya kuiondoa Marekani kutoka kwa shirika la afya duniani WHO, punde baada ya kuapishwa kwa Trump.
Israel Katz, Waziri wa Ulinzi wa Israel, amekiri kwamba Israel ilimuua aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wa Hamas Ismail Haniyeh.
Pandisha zaidi