Ghasia hizo zilisababisha shutuma kali za kimataifa pamoja na malalamiko ya mashambulizi ya makusudi dhidi ya Wayahudi, huku zikisababisha watu 5 kulazwa hospitali na wengine 20 kupata majeraha madogo. Zaidi ya watu 60 walikamatwa kufuatia ghasia hizo. Mashabiki wanaoiunga mkono Palestina waligombana na mashabiki wa Israel wakati wa mechi hiyo. Ghasia hizo zilikemewa kama vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi, huku waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiahidi kuwaondoa wafuasi wa Maccabi. Ghasia hizo zilizozua mjadala mkubwa kimataifa ziliharibu hadhi ya Uholanzi kama nchi yenye ustahmilivu kwa kila mmoja pamoja na Imani zao wakiwemo Wayahudi. Inaaminika kuwa ghasia hiyo zilichochewa zaidi na vita vinavyoendelea huko Gaza.
Forum