Bustan ya Manger imekosa mapambo yake ya kawaida sawa na kukosa watalii wanaotembelea sehemu hiyo wakati wa sherehe za krismasi.
Kuna hali ya utulivu na ukimya nje ya kanisa la Nativity lililojengwa mahali wakristo wanaamini kwamba ndipo alipozaliwa Yesu Kristo.
Vita na machafuko katika Ukingo wa Magharibi vimesababisha kutofanyika kwa sherehe za krismasi katika mji wa Bethlehem na hivyo kuathiri uchumi wa mji huo, ambao kwa kiwango kikubwa mapato yake – karibu asilimia 70 - yanategemea utalii wa krismasi.
Uchumi wa Ukingo wa Magharibi umeharibika sana kutokana na vizuizi dhidi ya wafanyakazi, ambao hawaruhusiwi kuingia Israel wakati huu wa vita.
Forum