Shirika rasmi la habari la IRNA, limesema kuwa wajumbe wa baraza hilo linaloongozwa na rais, wakiwemo spika, mkuu wa sheria pamoja na mawaziri kadhaa kwa kauli moja walipiga kura kuridhia hatua hiyo. Hata hivyo haiko bayana ni lini uamuzi huo utatekelezwa.
Marufuku hiyo ilizua mjadala mkali nchini Iran huku wakosoaji wa hatua hiyo wakidai kuwa udhibiti huo unakuja na gharama kubwa katika nchi.
“Marufuku hiyo haikuwa na faida yoyote, ila kusababisha ghadhabu na gharama kubwa kwa maisha ya watu,” mshauri wa rais Ali Rabiei amesema Jumanne, kupitia mtandao wa X.
Gazeti litolewalo kila siku la Shargh Jumanne, liliripoti kuwa wabunge 139 kati ya jumla ya 290 kwenye bunge la Iran waliandika barua kwa baraza hilo wakisema kuwa kuondolewa kwa marufuku ya WhatsApp, ni sawa na kuwapa zawadi maadui wa Iran.
Badala yake wabunge hao walipendekeza kuwepo na mitandao ya kijamii inayodhibitiwa ili kulinda sheria za kiislamu.
Forum