Ripoti mbalimbali nchini Tanzania zinaonyesha rushwa kubaki kuwa changamoto kubwa inayoathiri sekta nyingi nchini, huku vijana wakiathirika zaidi.
WHO ilisema kesi 406 za ugonjwa huo usiojulikana zilirekodiwa Oktoba 24 hadi Disemba 5 ambapo wagonjwa 31 walifariki.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumapili amesema kuwa kuanguka ghafla kwa serikali ya Syria ya Bashar al Assad ni “kitendo cha msingi cha haki,” lakini ni wakati wa kutokuwa na uhakika kwa Mashariki ya Kati.
Rais-mteule wa Marekani, Donald Trump ameapa kufanya mabadiliko makubwa na ya haraka baada ya kuchukua ofisi Januari 20, kwa kuwarudisha makwao mamilioni ya wahamiaji walio ndani ya nchi kinyume cha sheria.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump Jumapili ametoa wito wa sitisho la haraka la mapigano na mazungumzo kati ya Ukraine na Russia ili kumaliza “vita visivyo na maana”, na kupelekea Rais Volodomyr Zelenskiy kusema amani haiwezi kupatikana bila dhamana.
Vyanzo ndani ya makundi ya wanamgambo wa Palestina huko Gaza Jumapili vimesema kwamba Hamas imewataka kukusanya taarifa kuhusu mateka wanaoshikiliwa na makundi hayo kwa ajili ya maandalizi ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka na Israel.
Mtandao wa kundi la waokoaji wa kujitolea nchini Sudan umesema raia 28 wameuawa Jumapili wakati kituo cha mafuta kilichopo katika eneo la Khartoum chini ya udhibiti wa kundi la RSF kiliposhambuliwa kwa makombora.
Mgombea wa chama tawala nchini Ghana cha New Patriotic, Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia Jumapili amekubali kushindwa katika uchaguzi wa rais baada ya kushindwa kushughulikia kero kubwa ya wananchi kutokana na hali mbaya ya uchumi.
Serikali ya Syria inaripotiwa imepinduliwa mapema Jumapili na kufikisha kikomo kwa mshangao utawala wa miaka 50 wa familia ya Assad.
Mashambulizi ya Israel huko Gaza yameua watu 20 Jumamosi, maafisa wa afya wamesema, huku Qatar ikielezea matumaini ya kasi mpya katika juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas.
Watu 26 walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa siku ya Ijumaa katika ajali kati ya mabasi mawili madogo magharibi mwa Ivory Coast, wizara ya uchukuzi ilisema.
Pandisha zaidi